1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luanda. Viongozi watayarisha ulinzi wa mipaka.

23 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEYe

Afisa wa umoja wa mataifa amesema kuwa mataifa 11 ya Afrika yanayopanga mkutano ujao kuhusu eneo tete la maziwa makuu, uliopangwa kufanyika mwezi wa Desemba watakutana nchini Angola wiki ijayo kutayarisha mkataba juu ya ulinzi wa mipaka yao.

Mkutano wa matayarisho unaoanza Jumatatu, pia utajadili kuwalinda watu waliokimbia waeneo yao, na kuanzisha utaratibu wa kijimbo wa kulinda mali asili ili zisiweze kutumika katika kugharamia masuala ya vita, pamoja na demokrasia na utawala bora.