1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LONDON:Rais George W Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Uingereza

20 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFza
Tony Blair wamelaani vikali mashambulio mjini Istanbul. Wakikutana na waandishi wa habari mjini London, walielezea kuwa mapigano dhidi ya ugaidi wa kimataifa lazima kuendelea bila ya kigeugeu. Kuhusika na suala hili hakuna maridhiano wala kusita-sita. Bush alisisitiza wagaidi hawatafanikiwa kuzivunja nyoyo za Uingereza na Marekani. Wakati huo huo alitetea tena haja ya vita vya Irak. Marekani na washirika wake wataondoka nchini Irak iwapo Demokrasia imejengeka katika nchi hiyo. Kiasi watu laki moja wanatarajiwa kuandamana mjini London leo, kupinga siasa ya Marekani na Uingereza kuhusiana na Irak.