LONDON:Mazungumzo yatuama juu ya bajeti ya Umoja wa Ulaya.
27 Oktoba 2005Viongozi wa Mataifa ya Umoja wa Ulaya wamo katika mazungumzo juu ya bajeti ya Umoja huo na changamoto ya utandawazi katika mkutano wao usio rasmi unaofanyika nje ya mji wa London.
Katika mkutano huo wa siku moja,Kamishna wa Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso,ametoa mapendekezo ya kuwepo mkakati wenye masharti nafuu kwa jamii ya kisasa.
Mapendekezo yake pia yanajumuisha kuwepo na biashara huru kwa bidhaa na huduma,uwekezaji zaidi katika eleimu ya juu,utafiti na ugunduzi wa mambo mapya,halikadhalika kuundwa kwa mfuko utakaowasaidia wafanyakazi ambao watakuwa wamechishwa kazi.
Uingereza na Italia zimeonesha kuunga mkono mpango huo wa Bwana Barroso,lakini Ujerumani na Uholanzi wameonyesha mashaka juu ya mfuko wa utandawazi,kwa maelezo kuwa Umoja wa Ulaya hauwezi kumudu bajeti ya ziada.