1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza na Ufaransa zaahidi kupambana na ugaidi.

26 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEqh

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair na waziri mwenzake wa Ufaransa Dominique de Villepin wameeleza nia yao ya pamoja ya kupambana na ugaidi katika mazungumzo mjini London.

Uingereza na Ufaransa zitashirikana kwa karibu zaidi dhidi ya ugaidi kufuatia shambulio la mabomu mjini London , na wakabadilishana majina ya watuhumiwa wa imani kali ya Uislamu pamoja na taarifa nyingine.

Katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari, Blair ameahidi kutoyumba dhidi ya nadharia za magaidi. Kwa mara nyingine tena amekana kuwa vita vya Iraq vimeimarisha nia ya magaidi kuishambulia Uingereza .

Alikuwa akizungumzia kuhusu kura ya maoni iliyoandikwa katika gazeti la Daily Mirror ambapo imeelezwa kuwa Waingereza wengi wanaamini kuwa sera za nchi yao kuhusu Iraq ilikuwa ni sababu ya mapambano hayo ya magaidi dhidi ya mji wa London.