1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

London. Uingereza inasema itajaribu kutatua mzozo wake na wanachama wengine wa Umoja wa Ulaya wa bajeti hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

30 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CEyg

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Bwana Jack Straw amesema leo kuwa nchi yake inania ya kufanya juhudi za dhati katika kipindi hiki ambacho Uingereza itakuwa rais wa umoja wa Ulaya kutatua mzozo kati yake na wanachama wengine wa umoja huo kuhusu mipango yake ya matumizi.

Bwana Straw ameliambia bunge katika mkesha wa kuanza kwa kipindi cha urais wa Uingereza katika umoja wa Ulaya kuwa nchi hiyo inatambua jukumu lake na itafanya kila linalowezekana kufikia makubaliano ya matumizi ya hapo baadaye hadi mwishoni mwa mwaka huu.

Matumaini ya kufikiwa makubaliano ya matumizi kwa ajili ya kipindi cha mwaka 2007 – 13 katika mkutano uliofanyika mjini Brussels yalivunjika wiki mbili zilizopita wakati Uingereza ilipokataa kuacha kurejeshewa fedha inazotoa kwa bajeti ya umoja huo , bila kupata uhakikisho wa mabadiliko ya mpango wa ruzuku kwa wakulima.

Hali hiyo ya mkwamo iliongeza hali ya mzozo katika umoja huo baada ya wapiga kura nchini Ufaransa na Uholanzi kuikataa katiba ya Ulaya katika kura ya maoni mwezi uliopita.