1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LILONGWE :Wafanyikazi wa serikali wagomea kazi

9 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEcy

Takriban wafanyikazi elfu 4 wa serikali katika eneo la Lilongwe nchini Malawi wanaendelea kufanya mgomo na kusababisha kusimama kwa shughuli za serikali wakidai nyongeza za malipo ya uzeeni.

Chama cha wafanyikazi wa serikali nchini humo kinamtaka pia waziri wa fedha nchini humo Gooddall Gondwe ajiuzulu kwa kushindwa kufuata makubaliano yaliyoafikiwa mapema juu ya nyongeza ya malipo hayo.

Rais Bingu wa Mutharika amesema serikali yake haina fedha zakuongeza malipo ya wafanyikazi hao.

Kiongozi huyo wa Malawi ameanzisha mabadiliko makubwa ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na kupunguza matumizi ya serikali nchini humo ili kuwashawishi wafadhaili.