1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lewandowski atapata nafasi nyingine ya kushinda Ballon d'Or

Sylvia Mwehozi
3 Desemba 2021

Kocha wa Bayern Munich Julian Nagelsmann anaamini Robert Lewandowski atakuwa na nafasi nyingine ya kushinda Ballon d'Or baada ya kukosa tuzo hiyo iliyogubikwa na utata dhidi ya Lionel Messi wiki hii.

https://p.dw.com/p/43neJ
FC Bayern Muenchen | Robert Lewandowski
Picha: Sven Simon/imago images

Kocha wa Bayern Munich Julian Nagelsmann anaamini Robert Lewandowski atakuwa na nafasi nyingine ya kushinda Ballon d'Or baada ya kukosa tuzo hiyo iliyogubikwa na utata dhidi ya Lionel Messi wiki hii.

Mashabiki wengi na wachambuzi wamesema kufunga mabao 41 mwishoni mwa msimu wa Bundesliga, kulimfanya mchezaji huyo kutawazwa mchezaji bora wa dunia siku ya Jumatatu.

"Bado naamini ana uwezekano wa kushinda" alisema Nagelsmann wakati akizungumza na waandishi wa habari siku ya ijumaa kuelekea mchezo wake na Dortmund.

"Ni muhimu kwa upande mwingine, kukiri juu ya kukatishwa tamaa lakini kwa upande mwingine ni kupata nguvu kwake na kuwa na motisha kwa ajili ya mambo makubwa zaidi”.

Jarida la michezo la Ufaransa France Football, ambalo ndilo hutoa tuzo hiyo, limedokeza juu ya uwezekano wa kumtaja mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 kama mshindi wa 2020 kwa historia. "Kuna msemo wa kuvutia; mshindi wa kesho hujifunza kutokana na kushindwa leo" alisema Nagelsmann.

Lewandowski ana matumaini ya kutawazwa kwa mara ya pili mfululizo kama mchezaji bora wa mwaka wa shirikisho la soka duniani FIFA hapo Januari 17.