Lekerkusen yatamba katika michuano ya Ulaya
18 Februari 2011Yalikuwa ni mabao ya Eren Derdiyok,Gonzalo Castro na Sidney Sam aliyepachika mawili, yaliyoipatia ushindi mzito Leverkusen na kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.
Katika mechi nyingine za michuano hiyo ya kombe la Ulaya, timu nyingine ya Ujerumani, Stuttgart, ilichapwa mabao 2-1 na Benfica ya Ureno mjini Benfica.
Stuttgart ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Martin Harnik, kabla ya Benfica kusawazisha na kuongeza la pili. Hata hivyo, bao hilo la ugenini linaiweka katika nafasi nzuri Stuttgart ya kusonga mbele.
Ama Liverpool ilitoka suluhu bin suluhu na Sparta Prague mjini Prague, matokeo kama hayo pia yakijitokeza katika mechi kati ya Napoli ya Italia na Villarreal.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/Reuters
Mhariri:Othman Miraji