Lai: China kamwe haiwezi kuiwakilisha Taiwan
10 Oktoba 2024Haya ni kulingana na Rais wa Taiwan Lai Ching-te siku ya Alhamis huku hiyo hatua yake ya kuonekana kuuma na kuvivia ikiighadhabisha China.
Lai aliyeingia afisini mwezi Mei baada ya kuchaguliwa mwezi Januari, haungwi mkono na China ambayo inamuita "mtenganishi". Beijing inadai kuwa Taiwan ambayo ina utawala wa kidemokrasia iko chini ya himaya yake, mtazamo ambao Lai na serikali yake wanaukataa.
Akitoa hotuba muhimu ya taifa nje ya afisi ya rais mjini Taipei, Lai amesisitiza kwamba Jamhuri ya China - ambalo ndilo jina rasmi la Taiwan, na Jamhuri ya Watu wa China, hazitegemeani.
"Katika ardhi hii, demokrasia na uhuru vinakuwa na kustawi. Jamhuri ya Watu wa China haina haki ya kuiwakilisha Taiwan," alisema Lai.
Azma ya taiwan kutetea uhuru wake, kudumisha amani katika Ukanda wa Taiwan na kutafuta mazungumzo ya usawa na heshima na China, hivyo bado havijabadilika, aliongeza Lai.