1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

La Liga kumtambulisha mwamuzi wa kike msimu ujao

Sylvia Mwehozi
2 Julai 2019

Ligi ya Uhispania La liga kuanzia msimu ujao itakuwa kwa mara ya kwanza na mwamuzi wa kike, limetangza shirikisho la soka la Uhispania siku ya Jumanne. 

https://p.dw.com/p/3LTGX
Spanien Fußball Logo erste Liga La Liga Logo
Picha: picture-alliance/AA/B. Akbulut

Guadalupe Porras Ayuso aliye na miaka 32 ambaye kwa saa ni mwamuzi msaidizi, atakuwa mwanamke wa kwanza katika historia ya ligi hiyo kuchezesha michezo ya ligi kuu. "Mwamuzi msaidizi atakuwa mwanamke wa kwanza kuonekana katika ligi", ilisema taarifa ya RFEF. Mwamuzi mwingine wa kike Marisa Villa, alitanagzwa katika orodha ya La Liga mwaka 2007 lakini hakufuzu vipimo vinavyotakiwa katika kuchezesha mechi. Porras Ayuso amekuwa mwamuzi katika ligi ya daraja la pili ya wanaume Segunda kwa misimu miwili na kabla ya hapo alikuwa ligi ya daraja la tatu ya Uhispania. Kutangazwa kwake ni hatua muhimu sana kuelekea usawa wa kijinsia katikia soka la Uhispania.