Tatizo la usugu wa dawa, linalotokana na dawa kama za antibiotiki kushindwa kufanya kazi kikamilifu katika mwili wa binadamu, limeongezeka sana katika dunia ya sasa. Makala ya Afya Yako inaangazia tatizo hili kiundani, kwa kuzingatia kampeni ya Kijamii ya ufahamu wa matibabu ya Jamii Medical Awareness nchini Tanzania, yenye lengo la kupiga vita tatizo la usugu wa dawa.