Kura ya maoni yapigwa Zanzibar na Pemba
31 Julai 2010Matangazo
Chama tawala cha CCM na chama kikuu cha upinzani cha CUF, vinaunga mkono kura hiyo ya maoni na vimetoa mwito kwa wananchi kuipigia kura ya "ndio."
Kuambatana na muundo mpya wa serikali hiyo, Zanzibar itakuwa na rais alie na makamu wawili. Makamu wa kwanza wa rais atatoka katika chama kitakachoshika nafasi ya pili katika uchaguzi na makamu wa pili atatokea chama kitakachoshinda.Mawaziri watachaguliwa kwa kuzingatia misingi ya uwiano.
Iwapo kura hiyo itapitishwa,katiba ya Zanzibar itafanyiwa marekebisho, ili kufungua njia ya kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa kwa matayarisho ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanywa Oktoba 31 mwaka huu wa 2010.