Kundi la mwisho la askari wa Ufaransa laondoka Bangui
16 Desemba 2022Kundi la mwisho la wanajeshi wa Ufaransa waliotumwa kurejesha utulivu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati limeondoka jana Alhamisi baada ya kulegalega kwa mahusiano kati ya nchi hizo mbili kutona na kuimarika kwa ushirikiano baina ya serikali mjini Bangui na Urusi.
Askari 47 wa idara ya lojistiki waliondoka kwenye mji mkuu Bangui wakiabiri ndege chama C.130 wakiwa kundi la mwisho la wanajeshi 130 la wanajeshi wa Ufaransa kuondoka kwenye taifa hilo lnalokabiliwa na mzozo.
Ufaransa, mkoloni wa zamani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ilituma zaidi ya wanajeshi 1,600 kusaidia kurejesha utulivu nchini humo baada ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013 yaliyozusha vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika miaka ya karibu mivutano iliibuka kati ya Ufaransa na Jamhuri ya Afrika ya kati kutokana na kuongezeka kwa ushawishi wa kijeshi wa Urusi nchini humo.