1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kundi la G5 kuvunjwa rasmi

6 Desemba 2023

Wanachama wawili waliobaki wa Muungano wa Afrika Magharibi wa G5 wamesema wanaidhinisha kuvunjwa kwa kundi hilo lililoundwa kupambana na uasi wa itikadi kali.

https://p.dw.com/p/4ZplV
Sehemu ya kikosi cha G5 kwenye Ukanda wa Sahel ambacho sasa kinavunjwa.
Sehemu ya kikosi cha G5 kwenye Ukanda wa Sahel ambacho sasa kinavunjwa.Picha: Hans Lucas/IMAGO

Baada ya nchi nyingine tatu waasisi kujiondoa, nazo Chad na Mauritania zimesema katika taarifa kuwa zinafahamu na kuheshimu uamuzi wa uhuru wa Burkina Faso na Niger kuondoka katika muungano huo wa kijeshi, zikifuata nyayo za Mali.

Zimesema zitatekeleza hatua zote muhimu kwa mujibu wa mkataba ulioanzisha muungano wa G5.

Soma zaidi: Jeshi Burkina Faso lakemewa licha ya uungwaji mkono

Kundi hilo liliundwa mwaka wa 2014 lakini limepata matokeo machache tu.

Katika mwaka wa 2017, viongozi wa nchi hizo tano walikubaliana kuunda kikosi kazi cha pamoja cha kupambana na ugaidi kikiungwa mkono na Ufaransa.

Lakini watawala wa kijeshi wa Burkina Faso, Niger, na Mali wote wameituhumu Paria kwa kuwa na jukumu la kupitiliza baada ya miaka mingi ya kupelekwa vikosi vya Ufaransa kwenye nchi hizo.