1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yazifuta idara za uhusiano na Korea Kusini

16 Januari 2024

Korea Kaskazini imetangaza kuzifuta idara zote za taifa zinazosimamia mahusiano na taifa jirani la Korea Kusini, uamuzi unaodhihirisha ukubwa wa mvutano uliopo sasa baina ya madola hayo mawili hasimu.

https://p.dw.com/p/4bHmh
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.Picha: KCNA/REUTERS

Tangazo hilo limetolewa na shirika la habari la Korea Kaskazini likinukuu uamuzi uliofikiwa wakati wa kikao cha bunge lisilo na nguvu la nchi hiyo kilichofanyika jana.

Kwenye hotuba yake mbele ya wabunge, kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amesema hana dhamira tena ya kuendelea na juhudi za kutafuta upatanishi na Korea Kusini akiilaumu serikali mjini Seoul pamoja na Marekani kuwa chanzo cha  kuchochea uhasama kwenye rasi ya Korea.

Amesema imekuwa vigumu kwa Korea Kaskazini kutafuta suluhu ya amani na hata uwezekano wa kutimiza ndoto za kuungana tena na jirani yake Korea Kusini.