1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ushirikiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini matatani

16 Januari 2024

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un ametishia kuingia vitani na jirani yake Korea Kusini iwapo hata sentimita 0.001 ya ardhi yake itanyakuliwa.

https://p.dw.com/p/4bJ4G
Korea Kaskazini | Pyongyang | Kim Jong-un
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong UnPicha: KCNA/REUTERS

Kitisho hicho kinatokea wakati Pyongyang ikiyavunja mashirika yanayoshughulikia ushirikiano na mazungumzo kati yake na Korea Kusini.

Shirika la habari la Korea Kaskazini KCNA limeripoti kuwa, Kim Jong Un amesema hatotambua mpaka wa bahari kati ya nchi hizo mbili na amependekeza kufanyike mabadiliko ya katiba ili kuiruhusu nchi hiyo "kuikalia" Seoul.

Ama kwa upande wa Korea Kusini, Rais Yoon Suk Yeol ameliambia baraza lake la mawaziri kuwa, iwapo Korea Kaskazini itaendelea na uchokozi wake, basi nchi yake itajibu vikali na kuashiria uwezo mkubwa wa jeshi lake wa kukabiliana na vitisho vya aina yoyote.