1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Korea Kaskazini yarusha roketi lake angani

Charo Josephat/RTRE5 Aprili 2009

Hatua ya Korea Kaskazini inakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa

https://p.dw.com/p/HQOb
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong IIPicha: dpa

Maafisa wa Japan wanasema Korea Kaskazini imerusha roketi lake mapema leo kama ilivyotangazwa hapo awali. Roketi hilo liepitia anga ya Japan na kuelekea bahari ya Pacific. Waziri mkuu wa Japan, Taro Aso, amewaamuru maafisa wake kuchunguza hatua hiyo ya Korea Kaskazini na kumpa maelezo.

Korea Kaskazini imekosolewa vikali na Marekani na mataifa ya Asia. Korea Kusini imeieleza hatua ya Korea Kaskazini kuwa kitodno cha kutojali. Japna imesema sehemu ya chini ya roketi hilo imeanguka katika bahari ya Pacific, ishara kwamba Korea Kaskazini urushaji wa roketi hilo umefaulu.

Serikali ya mjini Pyongyang ilisema inataka kuweka satelaiti ya mawasiliano angani, lakini Japan, Korea Kusini na baadhi ya mataifa ya magharibi yanaamini hatua hiyo ya Korea Kaskazini ni njama ya kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu.

Obama und Klaus vor EU-USA-Gipfel in Prag
Rais wa Marekani Barack Obama (kushoto) akimsalimia rais wa Jamhuri ya Cheki Vaclav KlausPicha: AP

Korea Kaskazini imefanya jaribio lake wakati rais wa Marekani, Barack Obama, akiendelea na ziara yake barani Ulaya huko mjini Prague katika Jamhuri ya Cheki.

Hii leo kiongozi huyo anatarajiwa kutoa mwito kuhusu kuangamiza silaha za nyuklia duniani katika matamshi anayotumai yataupa nguvu ujumbe wake katika mzozo wa nyuklia wa Iran na Korea Kaskazini. Wapambe wa rais Obama wanasema kiongozi huyo atatoa hotuba muhimu katika ziara yake ya Ulaya mjini Prague itakayohusu usambazaji wa silaha za nyuklia.