1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kaskazini

Korea Kaskazini yafyatua makombora mawili ya masafa mafupi

1 Julai 2024

Jeshi la Korea Kusini limesema kwamba Korea Kaskazini imefyatua makombora mawili ya masafa mafupi huku moja likifeli siku moja baada ya Pyongyang kuonya kuhusu matokeo mabaya kufuatia mazoezi makubwa ya pamoja.

https://p.dw.com/p/4hj59
Watu wanatazama runinga inayoonyesha jaribio la kombora la Korea Kaskazini.
Watu wanatazama runinga inayoonyesha jaribio la kombora la Korea Kaskazini.Picha: Jung Yeon-Je/AFP/Getty Images

Msemaji wa jeshi la Korea kusini Lee Sung-jun amesema kombora la pili lilionekana kuruka isivyo kawaida katika hatua ya awali na kuongeza kuwa kama lingelipuka angani, athari zake na vifusi vingetua Korea Kaskazini.

Korea Kaskazini inashutumiwa kwa kukiuka hatua za udhibiti wa silaha kwa kusambaza silaha kwa Urusi kutumia katika vita vyake nchini Ukraine.

Soma pia: Wanajeshi wa Korea Kaskazini wavuka mpaka wa ulinzi mkali

Uhusiano baina ya nchi hizo mbili umefikia kiwango cha chini kabisa, huku Pyongyang ikizidisha majaribio yake ya silaha na kutuma maputo ya takataka dhidi ya jirani yake Seoul.

Pyongyang tayari ilirusha maelfu ya maputo yenye takataka katika kile ilichoita ni kulipizia kisasi hatua ya Korea Kusini ya kurusha maputo yaliyokuwa na karatasi zilizoandikwa propaganda za kuipinga serikali ya Korea Kaskazini.