1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Korea Kaskazini yafanya majaribio ya makombora mapya

3 Februari 2024

Korea Kaskazini imefanya majaribio ya aina mpya ya makombora yenye vichwa vikubwa pamoja na kombora la kukinga ndege, katika muendelezoo wa kuongeza mashaka kwa hasimu wake Korea Kusini.

https://p.dw.com/p/4c0Jt

Ripoti hiyo kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini, imetolewa siku moja baada ya Jeshi la Korea Kusini kusema liligundua Korea Kaskazini ikifanya mashambulizi kadhaa ya makombora katika eneo la bahari kutokea katika eneo la pwani yake ya magharibi.Hiyo ni mara ya nne kwa Pyongyang kufanya mashambulizi ya namna hiyo kwa mwaka huu wa 2024. Kiongozi wa Korea Kaskanzini Kim Jong Un amesisitiza jitihada zake  zakujengachombo cha kivita cha nyuklia katika kukabiliana na vitisho vinavyoongezeka vya Marekani, Korea Kusini na Japan.