1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kongamano la Yad Vashem dhidi ya chuki dhidi ya wayahudi

21 Januari 2020

Miaka 75 baada ya mauwaji ya halaiki ya wayahudi yaliyofanywa na wanazi, Holocaust, Wanasiasa kutoka mataifa 40 wanakutana Yad Vashem nchini Israel kwa kongamano kuhusu namna ya kukabiliana na chuki dhidi ya wayahudi

https://p.dw.com/p/3WZLC
Ausstellung "Survivors" in Essen Rede Naftali Fürst, Holocaust-Überlebender
Picha: picture-alliance/dpa/R. Vennenbernd

 

 

Mshambuliaji alitokea kwa nyuma. Alimvua kofia ya kiyahudi-Kippa, kijana mmoja aliyekua katika chumba cha kubadilisha nguo katika ukumbi wa mazowezi na kuitupa ndani ya debe la taka huku akimwita "we yahudi mchafu", Palastina huru". Kisa hicho cha hujuma dhidi ya wayahudi kimemfika kijana mmoja wa miaka 19 mwishoni mwa mwaka jana, katika mji wa Freiburg, kusini mwa Ujerumani. Ni mojawapo ya visa elfu kadhaa vya kihalifu vya chuki dhidi ya wayahudi vinavyoripotiwa kutokea kila mwaka nchini Ujerumani.

Chuki dhidi ya wayahudi haikuanza leo, ingalipo tangu zama za kale. Katika enzi hizi za sasa, wabaguzi na wafuasi wasiasa kali za kizalendo ndio wanaoeneza chuki dhidi ya wayahudi.

Mtindo huu mpya wa chuki dhidi ya wayahudi umefikia kilele chake kwa kuuliwa  wayahudi milioni kadhaa na wanazi wa Ujerumani barani Ulaya. Lakini hata baada ya mauwaji hayo ya halaiki ya wayahudi-Holocaust, bado kuna wanao otea wayahudi wenye nguvu ndio wanaoiendesha dunia, kwa namna hiyo wayahudi wanatukanwa na kushambuliwa. Chuki dhidi ya wayahudi zitamalizika lini?

Kambi ya maangamizi na mateso ya Auschwitz
Kambi ya maangamizi na mateso ya AuschwitzPicha: Reuters/K. Pempel

Kumbukumbu za Holocaust ndio njia bora ya kupambana na chuki dhidi ya wayahudi

 Arthur Bondarev ni yahudi na mfuasi wa itikadi kali.Yeye anasema ": "Kwa mtazamo wake wa kidini haamini kama hisia hizo zitamalizika. Pengine  siku ya kiama ikiwadia. Hata hivyo na hadi wakati huo  utakapowadia, ni jukumu la kila mmoja kupambana na hisia kama hizo za chuki dhidi ya wayahudi .Hata kama pengine hisia hizo za chuki dhidi ya wayahudi hazitokoma moja kwa moja, isimaanishe kwamba hatulazimiki kupambana nazo."

 

Arthur Bondarev na wengine kama yeye wanapambana na visa kama hivyo kila kukicha. Mapambano dhidi ya hisia za chuki dhidi ya wayahudi ni ya aina gani katika jukwaa la kimataifa la kisiasa, hilo litajulikana january 23 mjini Jerusalem pale, warithi wa viti vya wafalme, mawaziri wakuu na marais watakapokutana na kuhutubia. Kumbusho la mauwaji ya halaiki la Yad Vashem limewaalika viongozi hao kuhudhuria "kongamano la tano kuhusu Holocaust, kongamano litakalosimamiwa na rais wa Israel Reuven Rivlin.

Viongozi 40 wa taifa na serikali wameshasema watahudhuria kongamano hilo ikiwa ni pamoja na marais wa Urusi, na Ufaransa, Vladimir Putin na Emmanuel Macron, mwanamfalme wa Uingereza Charles, makamo wa rais wa Marekani Pence na rais wa shirikisho la jamhuri ya Ujerumani Frank-Walter Steinmeier.

Rais wa Poland Andzej Duda hatoshiriki katika kongamano hilo kutokana na mvutano kati ya nchi yake na rais wa Urusi Vladimir Putin. Kongamano hilo limepewa jina "Tukumbuke Holocaust, tupambane dhidi ya chuki dhidi ya Wayahudi."

Wataalam wengi wanakubaliana kumbukumbu za mauwaji ya halaiki ya wayahudi Holocaust ndio njia muhimu zaidi ya kupambana na hisia za chuki dhidi ya wayahudi.

 Na hilo bila ya shaka litadhihirika katika kongamano la Yad Vashem.