1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kofi Annan ataka mageuzi

14 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEuZ

New York:

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, anatilia mkazo kupanuliwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Amesema mjini New York kuwa kwa wakati huu muundo wa Baraza hilo siyo wa kidemokrasia. Kwa hiyo, lazima hali hiyo irekebishwe na kwenda sambamba na ukweli wa kisiasa wa karne ya 21. Nchi 53 za Afrika zilizo wanachama wa Umoja wa Mataifa zimetangaza kuwa zitawasilisha azimio lao kuhusu suala hilo juma hili. Kinachojadiliwa hivi sasa ni kuongezwa kwa idadi ya Wanachama wa kudumu wakiwa na kura za turufu hali kadhalika na idadi ya Wanachama wa kuzunguka. Balozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa amesema kuwa nchi yake ikishirikiana na Japan, Brazil na India itaendelea kupigania kuwa na viti vya kudumu licha ya upinzani wa nchi nyingine, Marekani imetangaza juzi katika Halmashauri Kuu ya Umoja wa Mataifa kuwa inapinga azma hiyo ya nchi nne.