1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kofi Annan aondolewa lawama.

30 Machi 2005

Hatimaye kashfa ya chakula kwa mafuta iliyokuwa inamkabili katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Anna imefutiliwa mbali.

https://p.dw.com/p/CHhB
Koffi Annan
Koffi AnnanPicha: AP

Hatimaye Kashfa iliyokuwa ikimkabili katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Kofi Annan ya kuwa na ushawishi mkubwa katika mpango wa mafuta kwa chakula imefutiliwa mbali. Masuali yaliyoibuka kuhusiana na mpango huo wa Iraq hata hivyo huenda ikatoa nafasi zaidi kwa wakosoaji wa Umoja wa Mataifa. Saumu Mwasimba anasimulia zaidi.

Ripoti iliyotolewa hapo jana kutokana na uchunguzi uliokuwa ukiongozwa na Paul Volcker ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa hazina ya Marekani haukuonyesha ushahidi wowote wa kwamba katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Annan alikuwa na ushawishi katika mkataba huo wa mpango wa kiasi cha dolla bilioni 67 kwa kampuni ya Uswissi iliyokuwa imemwajiri kazi mwanawe Annan Kojo.

Aidha ripoti hiyo pia inasema Kampuni hiyo ya Uswissi Cotecna pamoja na Kojo mwenye umri wa miaka 31 mwanabiashara wa Nigeria ,walimpotosha katibu mkuu Koffi Annan kutokana na uhusiano wake uliondelea na kampuni hiyo.

Lakini sio hilo tu,kwani ripoti hiyo pia inasema Annan pamoja na maafisa wa umoja wa mataifa walishindwa kufanya uchunguzi barabara kuhusiana na sakata hiyo na kwamba yeye pamoja na aliyekuwa mkuu wake wa watumishi wa umoja wa mataifa na pia swahibu yake wa

muda mrefu waliharibu stakabadhi muhimu kuhusiana na mpango huo.

Seneta wa Marekani Norm Coleman wa minnesota kutoka chama cha Repulican aliyemkosaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa alitaka Annan ajizulu kutoka Umoja huo mara moja.

Kutokana na kile alichokitaja senata huyo kuwa mambo yaliyochanganyikana ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uongozi ubinafsi na pia ukosefu wa uajibikaji ndicho kinachomfanya atake Annan Ajiuzulu.

Hata hivyo lakini ikulu ya White House imetoa sauti moja ya kumuunga mkono Katibu mkuu Annan na hata baadhi ya mataifa ya Ulaya pia yanatarajiwa kumuunga mkono bwana Annan ambapo tayari Ureno imetoa sauti ya kumuunga mkono . Lakini wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama China imesema huu ndio wakati muafaka wa suala hilo kujadiliwa kwa karibu.

Balozi wa China wa Umoja wa mataifa Wang Guangya amsema nchi yake imeshusha pumzi kutokana na kuondolewa lawama katibu mkuu Koffi Annan na hivyo anamini huu ndio wakati mzuri wa kuiondoa picha mbaya inayomzunguka Annan.

Kashfa hiyo inayohusu dolla bilioni 67 kwa ajili ya mpango wa chakula kwa mafuta iliiruhusu serikali ya Iraq chini ya uongozi wa Sadaam Hussein kuuza mafuta kwa kubalishana na chakula cha wananchi wanaoishi chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Mpango huo ulianza mwezi wa Desemba mwaka 1996 na kumalizika baada ya Marekani kuivamia Iraq katika mwaka 2003. Baad ya Iraq ikatoa stakabadhi zilizoonyesha ulaji Rusha,pamoja na wizi wa mafuta.

Ripoti hiyo mpya zaidi ilituwama juu katibu mkuu Annan na mwanawe Kojo. kampuni ya Uswissi ya Cotecna alikokuwa anafanya

kazi Kojo ilipokea kiasi cha dolla milioni 10 kila mwaka katika kandarasi ya Umoja wa Mataifa nchini Iraq.

Awali Kabla ya kutolewa kwa kandarasi hiyo katika mwaka 1998 Ripoti hiyo inaeleza Kofi Annan alikutana na maafisa wa kampuni ya Cotecna mara tatu lakini pia inaeleza kwamba haikudhibitishwa Annan alikuwa na ushawishi na kampuni hiyo ya Uswissi ambayo ilipanga mikutano hiyo.

Wakati Annan akiapa kwamba hatajiuzulu na ataendelea na mpango wake wa kuleta mageuzi katika Umoja huo, Marekani imesema kwamba iko tayari kuunga mkono juhudi zake hizi Annan za kuleta mageuzi katika Umoja wa mataifa.

Ripoti hiyo ya Jopo la Volker ni ya pili kuchunuza madai ya ufisadi katika Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo imeilemea sana kampuni ya Cotecna na mwanawe Annan Kojo ikieleza walijaribu kuficha uhusiano wao baada ya kampuni hiyo kupewa kandarasi hiyo na kwamba Kojo alimpotosha babake.

Ripoti ya mwisho hata hivyo itatolewa mwezi Juni na mara hii ripoti hiyo itajumuisha pamoja na vitendo vya wanachama 15 wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.