1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bazoum pamoja na familia yake wanaendelea vizuri

23 Oktoba 2023

Duru zilizoko karibu na raisi aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum zimesema, yeye na familia yake wanaendelea vizuri baada ya utawala wa kijeshi nchini humo kudai wiki iliyopita kwamba alijaribu kutoroka.

https://p.dw.com/p/4Xtwx
Kiongozi wa Niger alieondolewa madarakani Mohamed Bazoum
Kiongozi wa Niger alieondolewa madarakani Mohamed BazoumPicha: Stevens Tomas/ABACA/IMAGO

Duru kutoka ndani ya familia zimesema kiongozi huyo aliruhusiwa pia kufanya mawasiliano ya simu na daktari wake aliruhusiwa kumuona na kumletea chakula.

Alhamisi iliyopita, msemaji wa utawala wa kijeshi uliomuondoa madarakani Bazoum alidai kwambakiongozi huyo wa zamani alikuwa anataka kutorokea Nigeria kwa kutumia helikopta ambayo ni mali ya mataifa makubwa ya nje.

Soma pia:Bazoum yupo salama - jamaa

Utawala huo uliongeza kuwa wahusika wakuu na washirika wao kwenye mpango wa kumtorosha Bazoum wamekamatwa.