1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan ziarani nchini Uganda

16 Septemba 2023

Kiongozi wa kijeshi wa Sudan, Abdel Fattah al Burhan, leo anaelekea nchini Uganda kwa ziara itakayojumuisha mazungumzo na Rais Yoweri Museveni katika wakati mapigano bado yanaendelea mjini Khartoum.

https://p.dw.com/p/4WPuh
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan, Abdel Fattah al Burhan.
Kiongozi wa kijeshi wa Sudan, Abdel Fattah al Burhan.Picha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Baraza la Utawala wa Sudan limesema, viongozi hao watajadili juu ya ushirikiano na masuala yenye umuhimu kwa mataifa hayo mawili.

Hiyo ni ziara ya sita ya al-Burhan tangu alipojitokeza hadharani mwezi uliopita baada ya kupotea machoni mwa umma katikati ya mapigano makali yaliyoshuhudiwa mjini Khartoum. Miongoni mwa mataifa ambayo tayari ameyatembelea ni pamoja na Misri, Sudan Kusini na Uturuki.

Sudan imekuwa katika machafuko tangu mapigano yalipoibuka mwezi Aprili kati ya jeshi rasmi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan dhidi ya kikosi kilichoasi cha RSF chini ya aliyekuwa msaidizi wake Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.

Kwa mujibu wa shirika linalofuatilia mizozo na kukusanya taarifa la "Armed Conflict Location & Event Data Project" takribani watu 7,500 wameuwawa tangu mgogoro ulipoibuka nchini humo Aprili 15.