1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KINSHASA: Ugonjwa wa ebola wazuka

11 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQu

Maafisa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamesema matokeo ya mahabara yamethibitisha kuwa ugonjwa uliozuka kusini mashariki mwa nchi hiyo ni homa ya ebola.

Waziri wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Makenge Kaput, amesema taasisi ya kupambana na kuenea kwa magonjwa ya Atlanta nchini Marekani na mahabara ya nchini Gabon zimethibitisha kuwa ugonjwa huo ni ebola, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Watu zaidi ya 160 wamekufa kutokana na ugonjwa huo katika wilaya zilizoathirika za Mweka na Luebo tangu mwishoni mwa mwezi Agosti. Watu wengine takriban 400 wameambukizwa ugongwa huo wa ebola.

Ugonjwa wa ebola ulizuka mara ya mwisho nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo mwaka wa 1995 huko Kikwit ambapo watu 245 walifariki dunia.