1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kim Jong Un aombwa kuzungumza na mrithi wake Suk Yeol

22 Aprili 2022

Rais wa Korea Kusini Moon Jae In amemtolea mwito kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, kuingia kwenye mazungumzo na serikali ya mrithi wake, Yoon Suk Yeol.

https://p.dw.com/p/4AI5j
Nordkorea | Südkorea | Moon Jea-In trifft Kim Jong-Un beim Inter-Korea-Gipfel 2018
Picha: Inter-Korean Press Corps/ZUMAPRESS/picture alliance

Ofisi ya rais mjini Seoul imeeleza kwamba katika barua yake ya kuaga, Rais Moon pia ameelezea matumaini yake kwamba serikali ya mjini Pyongyang huenda hivi karibuni ikarudi kwenye mazungumzo na Marekani kuhusu mpango wa nyuklia wa nchi yake, mazungumzo ambayo hadi sasa yamekwama.

Aidha, kwa upande mwingine, imeelezwa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, amemshukuru rais huyo anayeondoka wa Korea Kusini kwa kujaribu kuimarisha mahusiano. 

Hatua hiyo ya Kim Jong Un, ambayo sio ya kawaida ya kuonesha nia njema, imeelezwa na wachambuzi kwamba haitoshi kumaliza mvutano unaoongezeka kati ya Korea hizo mbili. 

Kufuatia majaribio chungu nzima ya makombora mwaka huu, Marekani na Korea Kusini zinahofia Korea Kaskazini huenda hivi karibuni ikafanya jaribio jingine la silaha za nyuklia.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW