1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiTunisia

Mamlaka nchini Tunisia yawaokoa wahamiaji 34

16 Machi 2024

Mamlaka nchini Tunisia imewaokoa wahamiaji 34 na miili ya watu wawili iliyokutwa katika pwani ya kusini mashariki mwa nchi hiyo jana Ijumaa.

https://p.dw.com/p/4dnID
Mediterania | Meli ya uokozi ya Watch 5
Picha hii iliyotolewa na shirika la usaidizi la Sea-Watch inaonyesha wafanyakazi wa "Sea-Watch 5" wakiwaokoa watu waliomo kwenye mashua ya mbao iliyofurika na ambayo ilipigwa na mawimbi katika bahari ya MediteraniaPicha: Maria Giulia Trombini/Sea-Watch/dpa/picture alliance

Taarifa ya Walinzi wa Kitaifa imesema kuna uwezekano kwamba watu wengine 34 wamepotea, baada ya manusura kuwaarifu kwamba kulikuwa boti waliyoipanda ilikuwa imewabeba watu 70 kabla ya kupinduka.

Walinzi hao wamesema bado wanawatafuta watu waliopotea.

Tunisia na Libya zimekuwa zikitumiwa kwa kiasi kikubwa na wahamiaji wanaoondoka Afrika, ambao hupita njia hatari ya bahari wakikimbilia Ulaya kutafuta maisha bora kila mwaka .

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM limesema watu 2,498 walikufa au kupotea walipokuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania mwaka uliopita, ikiwa ni ongezeko la asilimia 75 ikilinganishwa na mwaka 2022.