1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kigali. Mawaziri wa kilimo wa Afrika wataka kuimarishwa zaidi ulinzi dhidi ya virusi vya homa ya ndege.

5 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CELk

Afrika itahitaji msaada wa kifedha na utaalamu wiki ijayo katika mkutano mjini Geneva ambao utajadili upatikana wa fedha duniani pamoja na mikakati ya kupambana na virusi hatari vya homa ya mafua ya ndege.

Mawaziri wa kilimo kutoka mataifa 17 ya Afrika pia wametoa wito kwa bara hilo kuimarisha uwezo wake wa kuchunguza virusi hivyo mwishoni mwa mkutano wao uliofanyika katika mji mkuu wa Rwanda , Kigali , uliopewa jukumu la kutafuta njia ya kupambana na kitisho hicho katika eneo hilo la dunia.

Mkutano huo umeyataka mataifa ya Afrika kuimarisha uwezo wake katika nyanja ya uchunguzi wa virusi hivyo vya mafua ya ndege pamoja na kuweka tayari fedha za dharura.

Virusi hivyo vya H5N1 havijapatikana katika ndege barani Afrika lakini wataalamu wanasema upatikanaji pamoja na udhibiti wa virusi hivyo inaweza kuwa kazi kubwa sana iwapo vitaingia katika maeneo ya vijijini katika bara hilo.