1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEL:Peter Harry Castensen ndie waziri mkuu mpya wa jimbo la Schelswig-Holstein

27 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFIm

Peter Harry Castensen sasa ndiye waziri mkuu mpya wa serikali ya jimbo la Schleswig-Holstein.

Chama cha Christian – Demokrat kilichaguliwa na kura 54 kati ya kura 69 za bunge mjini Kiel.

Harry anaongoza serikali ya muungano wa vyama vikuu viwili Demokratic Union na Social Demokratic Party.

Vyama hivyo viwili viliunda serikali ya muungano mapema mwezi huu kufuatia kushindwa kwa jaribio la waziri mkuu wa zamani wa jimbo hilo bibi Heide Simonis la kuunda serikali

Katika uchaguzi wa Februari chama cha Social Demokrats kilishindwa kwa nafasi moja ya kiti na chama cha Christian Demokrats,lakini Bibi Simonis alijaribu kutaka uongozi kupitia usaidizi wa chama cha kijani na SSV,na chama cha jumuiya ya Waden walioko katika jimbo hilo. Jaribio hilo lilishindwa baada ya mbunge mmoja kukataa kupigia kura ya kumuunga mkono bungeni.