1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya yaongoza riadha Afrika, yamaliza ya 5 duniani

28 Agosti 2023

Kenya imemaliza mashindano ya dunia ya riadha huko Budapest Hungary, Jumapili, katika nafasi ya 5 katika jedwali la medali ikiwa na jumla ya medali 10 dhahabu zikiwa 3 fedha 3 na shaba 4.

https://p.dw.com/p/4Vetc
Faith Kipyegon (Goldmedaille in Budapest im 1.500m Lauf)
Bingwa wa mita 1500 na 5000 Faith Kipyegon wa KenyaPicha: imago images

Kenya ilipata dhahabu zake kupitia Faith Kipyegon aliyeshinda mbio za mita 1500 na 5000 halafu Jumapili dhahabu ya tatu ikatoka kwa Mary Moraa aliyeibuka kidedea katika mbio za mita 800.

Kipyegon ambaye anasubiriwa na wengi kuona iwapo kama mpinzani wake mkuu Sifan Hassan wa Uholanzi atajitosa katika kushiriki mbio za mita 10,000 hasa katika mashindano hayo ya Olimpiki, alisema haya baada ya kushinda dhahabu yake ya pili.

Tokyo 2020 | Sifan Hassan
Mwanariadha wa uholanzi Sifan HassanPicha: Matthias Schrader/picture-alliance/dpa

"Kina dada wenzangu walikuwa na nguvu bado na sote tulijua tunashindania dhahabu ila ilibidi nijiamini kwamba mimi ndiye ninayeishikilia rekodi ya dunia na kwamba Sifan yuko hapa na mimi, ilibidi tu nijisukume zaidi hadi mwisho," alisema Kipyegon.

Ethiopia imeshikilia nafasi ya sita ikiwa na jumla ya medali 9 halafu Uganda iliyonyakua medali mbili za dhahabu imemaliza katika nafasi ya tisa.

Vyanzo: Reuters/DPAE