1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
BiasharaKenya

Kenya yaanza kusafirisha maua na matunda Ulaya kwa meli

24 Mei 2023

Kenya imeanza kusafirisha bidhaa za matunda, mboga na maua hadi Ulaya kwa kutumia meli badala ya ndege.

https://p.dw.com/p/4RkHy
Kenia | Hafen in Mombasa
Picha: Joerg Boethling/IMAGO

Hatua hiyo inajiri siku 7 baada ya Umoja wa Ulaya kufikia makubaliano na serikali ya Kenya na wadau kukumbatia usafiri wa majini.

Makubaliano haya yanatekelezwa chini ya mpango wa miaka mitano wa kuimarisha mazingira ya biashara na kusafirisha bidhaa nje kati ya Umoja wa Ulaya na Kenya.

Dhamira ni kupunguza hewa ukaa na kuiongezea sekta hiyo mapato.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, kiongozi wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya nchini Kenya, Henriette Geiger, alisisitiza kuwa makubaliano hayo yanaendana na mkataba wa EU wa kulinda mazingira unaodhamiria kuifanya biashara kuwa endelevu na inayopunguza hewa ukaa.

Kenya ilijikusanyia pato la dola milioni 152.3 katika mwaka wa 2022 kupitia biashara ya kuuza nje mboga, matunda na maua.