1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Kaimu afisa mkuu mtendaji wa Kenya Airways atangazwa

16 Desemba 2019

Kenya Airways latangaza kaimu mtendaji mkuu atakayeliongoza shirika hilo kwanzia Januari. Hii ni baada ya aliyekuwa mtendaji mku kujiuzulu.

https://p.dw.com/p/3UtOF
Kenya Airways Boeing 737-800, vermisstes Flugzeug
Picha: AP

Shirika la ndege la Kenya limetangaza kumpata kaimu mtendaji mkuu atayaeanza kazi Januari mwaka unaokuja baada ya mtangulizi wake kujiuzulu mnamo mwezi Mei kufutuia mpango wa kutaifishwa tena shirika hilo lilinalokabiliwa na hasara.

Kiongozi huyo mpya Allan Kilavuka ambaye hivi sasa ni mtendaji mkuu wa kampuni tanzu ya Kenya Airways iitwayo Jumbojet atahudumu katika nafasi hiyo kama kaimu hadi pale shirika hilo la ndege litakapomteua mtendaji mkuu wa kudumu.

Mwezi Julai wabunge nchini kenya walipiga kura kuirejesha Kenya Airways chini cha udhibiti wa serikali iliyokuwa ikimiliki asilimia 48.9 ya hisa.

Mtendaji mkuu anayeondoka Sebastian Mikosz alitangaza mipango yake ya kuachia wadhifa huo mapema mwaka unaokuja kwa sababu binafsi baada ya kuliongoza shirika hilo tangu mwezi Juni 2017.

Mwezi Agosti mwaka huu Kenya Airways ilirekodi hasara ya shilingi za Kenya bilioni 8.56 kiwango ambacho ni maradufu ya hasara iliyopatikana mwaka uliopita.