SiasaKazakhstan
Kazakhstan yapiga kura ya kujenga mtambo wa nyuklia
6 Oktoba 2024Matangazo
Kazakhstan imeanza kupiga kura ya maoni siku ya Jumapili kuhusu iwapo ijenge mtambo wake wa kwanza wa nyuklia, wazo lililokuzwa na Serikali ya Rais Kassym-Jomart Tokayev.
Mpango huo umekabiliwa na ukosoaji wa umma juu ya wasiwasi wa hatari zinazohusiana na matumizi ya nyuklia, majaribio yake na hofu kwamba Urusi itashiriki katika mradi huo.
Katika kijiji cha Ulken mwambao wa Ziwa Balkash, ambayo baraza la mawaziri limeteua kama mahali pa kujenga kinu hicho, baadhi ya wenyeji wanatarajia mradi huo kubuni nafasi za ajira, huku wengine wakielezea wasiwasi wao kuhusu athari katika ubora wa maji ya ziwa.
Kazakhstan inaagiza umeme, kutoka Urusi, kwasababu vifaa vyake vingi ni vya zamani na vinashindwa kukidhi mahitaji ya ndani.