1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

UN yataka usafirishaji haraka wa nafaka kutoka Ukraine

21 Juni 2023

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa mwito wa kuharakishwa usafirishaji wa nafaka kutoka bandari za Ukraine zilizopo kwenye bahari nyeusi kama ilivyokubaliwa chini ya mkataba uliopo.

https://p.dw.com/p/4Ss5J
Kenia l UN Generalsekretär Antonio Guterres in Nairobi
Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Mkataba huo uliofikiwa mwaka uliopita kati ya Urusi na Ukraine chini ya upatanishi wa Umoja wa Mataifa na Uturuki, uliruhusu usafirishaji nafaka kwa lengo la kupunguza mzozo wa chakula duniani uliochochewa na uvamizi wa Moscow nchini Ukraine.

Shehena inayosafirishwa hivi sasa imepungua kutoka tani milioni 4.2

Hata hivyo shehena ya chakula inayosafirishwa hivi sasa imepungua kutoka tani milioni 4.2 mnamo Okotba mwaka jana hadi tani milioni 1.3 pekee mwezi Mei mwaka huu. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq amesema katibu mkuu Guterress anafadhishwa na hali hiyo na amezihimiza pande zote kufanya kila linalowezesha kuhakikisha makubaliano yaliyofikiwa yanatekelezwa kikamilifu.