1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KASHMIR. Wahanga wa tetemeko la ardhi wapokea misaada

9 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEK9

Pakistan na India zimefungua kizuizi cha pili katika mpaka wao ili kuwezesha misaada ya kibinadamu kuwafikia wahanga wa tetemeko la ardhi la oktoba 8 huko kusini mwa Asia.

Lakini amri ya kutowaruhusu wakashmiri kuvuka mpaka huo bado inadumishwa.

Pande zote mbili zinatarajiwa kuanza kuwaruhusu watu wake kuvuka mpaka huo mara tu taratibu zote zitakapo kamilika.

Wanajeshi na maaafisa wa shughuli za kutoa misaada walionekana wakipokezana magunia ya vyakula, Mablanketi na nguo kutoka India na pakistani kwa ajili ya wahanga hao.