1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

Kashmir kuandaa uchaguzi wa serikali za mitaa

16 Agosti 2024

Majimbo ya Jamuu na Kashmir yaliyo chini ya utawala wa India, yatafanya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mara ya kwanza katika muda wa muongo mmoja.

https://p.dw.com/p/4jYuE
Indien | Parlamentswahlen 2024 | Wähler in Kaschmir
Picha: Salahuddin Zain/DW

Hii ni baada ya uchaguzi kusimama katika eneo hilo linalozozaniwa kufuatia hatua ya India kufuta hadhi maalum ya jimbo hilo mnamo mwaka 2019.

Zoezi la uchaguzi litafanyika katika awamu tatu kati ya Septemba 18 na Oktoba 1.

Tume ya uchaguzi imesema jumla ya watu milioni 8.7 wamesajiliwa kupiga kura katika eneo hilo.

India na Pakistan zinadhibiti maeneo tofauti ya jimbo la Kashmir lakini nchi zote mbili zinadai umiliki kamili wa jimbo hilo lenye waislamu wengi tangu ilipojipatia uhuru wake kutoka Uingereza mwaka 1947.