1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiNigeria

Watu wasiopungua 59 wafariki kwa moto nchini Nigeria

9 Septemba 2024

Watu wasiopungua59 wamekufa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na lori la mafuta na kulipuka katika jimbo la Niger huko kaskazini mwa Nigeria.

https://p.dw.com/p/4kQSO
Moja ya barabara zilizoharibika nchini Nigeria
Ajali za barabarani nchini Nigeria pamoja na mambo mengine husababishwa na barabara mbaya ambazo hazikarabatiwi mara kwa maraPicha: Ayodeji Oluwagbemiga/REUTERS

Msemaji wa shirika la dharura wa eneo hilo Ibrahim Husseini, amesema idadi ya waliokufa katika ajali hiyo iliyotokea Jumapili asubuhi imeongezeka na kufikia 59, kutoka 52 za mapema Jumatatu na tayari wamezikwa.

Katika ajali hiyo, ng'ombe 50 pia waliungua kwa moto baada ya lori la mafuta.

Milipuko ya malori yanayobeba mafuta imekuwa ikitokea mara kwa mara Nigeria ambapo barabara za taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika hazifanyiwi ukarabati ipasavyo.

Wakati wa ajali za aina hiyo, wakaazi wa maeneo kunakotokea hukimbilia kukinga mafuta kutoka kwenye malori hayo.