1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSomalia

Karibu watu 20 wauawa Somalia

2 Januari 2023

Watu wapatao 20 wameuawa katika eneo lililojitenga na Somalia, Somaliland kwenye mapigano kati ya waandamanaji wanaoipinga serikali na vikosi vya usalama vya serikali.

https://p.dw.com/p/4LdSW
Somaliland I Großbrand auf dem zentralen Markt in Hargeisa
Picha: Mataan Yuusuf/AFP/Getty Images

Hayo ni kwa mujibu wa daktari katika hospitali ya umma.

Mohamed Farah, daktari katika hospitali ya umma ya Laascaanood, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa takriban watu wengine kadha wamejeruhiwa. Amesema ameiona miili ya waliofariki iliopelekwa katika hospitali hiyo.

Waandamanaji wanaitaka Somaliland kuacha udhibiti wa mji huo na pia wamevishtumu vikosi vya usalama kwa kushindwa kumaliza visa vya ukosefu wa usalama katika mji huo.

Kwa zaidi ya wiki moja, vikosi vya usalama vimekuwa vikipambana na waandamanaji huko Laascaanood, mji wa mashariki mwa Somaliland ambao unagombaniwa kati ya mamlaka ya Somaliland na jirani yake Puntland, mojawapo ya mikoa yenye mamlaka yake ya ndani.