1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampuni ya Bavarian Nordic kutengeneza dozi 440,000 ya mpox

22 Agosti 2024

Kampuni ya Denmark ya kutengeneza dawa ya Bavarian Nordic imetia saini mkataba wa kusambaza dozi 440,000 ya chanjo dhidi ya homa ya nyani kwa "nchi moja ya Ulaya ambayo haikutajwa."

https://p.dw.com/p/4jmQk
Denmark | Bavarian Nordic | Mtaalamu wa dawa na chango
Mtaalamu kutoka kampuni ya Denmark ya kutengeneza dawa ya Bavarian NordicPicha: Bavarian Nordic/abaca/picture alliance

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Paul Chaplin amesema maombi ya kusambaza dozi hizo za chanjo yalijumuishwa kwenye makadirio yake ya mwaka huu.

Wiki iliyopita, kampuni hiyo ilisema iko tayari kutengeneza chanjo hadi dozi milioni 10 ya mpox ifikapo mwisho wa mwaka 2025.
Shirika la afya duniani WHO limetoa wito wa kutengenezwa kwa chanjo zaidi huku kipaumbele ikiwa kwa nchi zilizoathirika zaidi na ugonjwa huo wa homa ya nyani.

Soma pia: Tanzania yaanza ufuatiliaji ili kuzuia maambukizi ya Mpox
Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika, kimeeleza kuwa dozi 20,000 za chanjo zitasambazwa kote barani Afrika, kufuatia makubaliano kati ya Umoja wa Ulaya na kampuni ya kutengeneza dawa ya Bavarian Nordic.