1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kamati ya baraza la Senet inawatuhumu wanasiasa wawili,wa Uengereza na Ufaransa kuhongwa zamani na Sadam Hussein

12 Mei 2005
https://p.dw.com/p/CFE8
Kamati ya baraza la Senet la Marekani inadai kwamba mbunge wa Uengereza George Galloway na waziri wa zamani wa mambo ya ndani wa Ufaransa,Charles Pasqua walipatia vibali na Sadam Hussein chini ya mpango wa umoja wa mataifa wa mafuta kwa chakula.Kwa namna hiyo mafuta yaliweza kuuzwa kinyume na mpango wa umoja wa mataifa.Ripoti ya kamati ya baraza la Senet la Marekani haijatoa ushahidi wowote kwamba wanasiasa hao walipokea fedha.Wote wawili wamekanusha tuhuma hizo.Kamati ya baraza la Senet la Marekani inasema nyaraka za wizara ya mafuta ya utawala wa zamani wa Sadam Hussein pamoja na mahojiano yaliyofanywa pamoja na afisa wa ngazi ya juu wa utawala huo wa zamani.Mpango wa mafuta kwa chakula wa Umoja wa mataifa ulilengwa kuwapunguzia shida wananchi wa Irak waliokua wakisumbuliwa na vikwazo vya kiuchumi vya kimataifa.Mpango huo ulisitishwa baada ya vikosi vinavyoopngozwa na marekani kuingia Irak mnamo mwaka 2003.