Guinea: Jumba la makumbusho la utamaduni wa Peul
3 Desemba 2015Matangazo
Zeinab Koumanthio Diallo ni mshairi wa Peul na mkurugenzi wa jumba pekee la makumbusho nchini Guinea linalohifadhi utamaduni wa Peul. Miaka kumi iliyopita, baada ya kufanya kazi na mashirika ya kimataifa na kufanikiwa kama mwandishi, alirejea nyumbani kwao katika eneo la Futa Jallon, katikati ya Guinea. Tangu wakati huo, amekuwa akieneza utamaduni wa Peul, kabila la wafugaji wa kuhamahama. Diallo alijenga jumba la makumbusho mjini Labe, ambako vitu vya kale vya kabila la Peul vinahifadhiwa. Kwa sasa, jumba hilo lilibadilishwa kuwa kituo cha utamaduni wa jadi. Zeinab Koumanthio Diallo ameanzisha klabu ya majadiliano ya vitabu na anajaribu kuwavutia vjana katika tamaduni za Peul.