1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Julai 20,1944 jaribio la kumuua Hitler

19 Julai 2007

Siku hii,miaka kiasi ya 60 iliopita, lilifanyika jaribio la kumuua Adolf Hitler ambalo lilishindwa.Athari zake lakini zilikuwa kubwa.

https://p.dw.com/p/CHAo

Julai 20 ni siku inayokumbukwa kama siku lilipofanyika jaribio,1944 kumuua kwa mripuko wa bomu Adolf Hitler katika makao makuu yake huko “Wolfsschanze” karibu na Rastenburg,mashariki mwa Prussia.Akiamini kuwa jaribio lake la kumuua Hitler limefanikiwa,Claus Schenk Graf von Stauffenberg,alirejea Berlin,mji mkuu.

Ilipodhihirika dhahiri-shahiri kuwa Hitler alinusurika,njama nzima ya kumuangusha Hitler na utawala wake, ikaporomoka.Bila kupita muda -usiku wa Julai 21,1944 -von Stauffenberg na wenzake 3 walipigwa risasi na kuuliwa.

“Limefanyika hii leo jaribio la kumuua Kiongozi Adolf Hitler.Mbali na majaraha madogo, amenusurika na maisha.Bila ya kuchelewa,Kiongozi ameendelea na shughuli zake na kama ilivyopangwa amekutana na Duce-kiongozi wa Itali- Mussolini kwa mazungumzo marefu.”

Baada ya taarifa ya jaribio hilo la kumuua Hitler kuenea katika milki ya Ujerumani, wasikilizaji katika radio hawakuamini moja kwa moja kuwa lilifanyika jaribio la kumuua adolf Hitler.Yule lakini aliekuwa na shaka shaka,siku moja baadae Julai,21,1944 alipewa ushahidi kuwa Hitler kweli alivuka salama katika njama ile ya kumripua kwa bomu lililopachikwa katika mkoba na kutegwa chini ya meza.

Hitler binafsi:

“Kikundi kidogo kabisa cha wenye uchu wa madaraka,kisicho na hisia wala busara,cha wahalfu -maafisa wapumbavu kilipanga njama ya kunihilikisha mimi na uongozi mzima wa jeshi la Ujerumani.”

Hitler akatangaza kwamba walioandaa njama hiyo hawataonewa huruma.Claus schenk Graf von Stauffenberg na wenzake 3 kwa hivi sasa tayari wameshanyongwa.

Ushujaa wa kuonesha upinzani dhidi ya utawala wa Hitler walikuwanao wachache tu.Miongoni mwao alikua afisa wa kijeshi Ewald-Heinrich von Kleist, ambae baba yake alikuwamo katika njama ya kumuua Hitler na alinyongwa na Manazi.Kijana von Kleist,alivuka salama akihurumiwa kunyongwa ingawa alishiriki katika patashika ya kuandaa jaribio la kumhilikisha Hitler.

Akiwa miongoni mwa wale wachache tu waliovuka na maisha kati ya walioshiriki kwenye njama ile,1994 alizungumza kwenye TV katika mwaka wa 50 kukumbuka mkasa ule:

“Ikinikereta mno kuona uhalifu uliopitishwa na dhulma ukifanyika kwa niaba ya wajerumani.Nikajiambia-hakuna njia ya kuonesha ulimwengu kuna Ujerumani yenye sura nyengine.Sababu ya pili ambayo ilikua muhimu kwangu ni kuwa:niliamini sana tukijaribu kumhilikisha Hitler,tungeokoa maisha ya wengi.Na hii kwangu, ilikua muhimu sana kuona Ujerumani haiteketezwi nmmna ile.”

Lakini katika propaganda ya vyombo rasmi vya dola,njama ya Julai 20,1944 ya kumuua Hitler, ilielezwa ni jaribio la wafamaji na la wachache kubadili mkondo wa mambo.

Ukweli wa mambo lakini, Hitler na wakereketwa wenzake wa kinazi wakihofia kupungua kwa ari ya kupigana katika majeshi ya Ujeruma