1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHN GARANG AKUTANA NA KOFI ANNAN

25 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFyL
NEW YORK: Kiongozi wa waasi nchini Sudan,John Garang amemuarifu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan juu ya maendeleo yaliopatikana kuhusu majadiliano ya amani ya Sudan.Garang ameeleza kwa urefu juu ya mipango ya usalama iliyokubaliwa.Annan kwa upande wake amethibitisha utayarifu wa Umoja wa Mataifa kuisaidia Sudan kukamilisha hatua za mwisho za makubaliano ya amani.Vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Sudan vilizuka mwaka 1983 baada ya chama cha SPLA cha John Garang kusini mwa nchi,kunyanyua silaha katika juhudi ya kutaka kukomesha utawala wa watu wa kaskazini ambao wengi wao ni waislamu.Katika eneo la kusini la Sudan wengi ni ama wakristo au hawana dini.Vita hivyo vimepoteza maisha ya watu milioni moja na nusu na wengine milioni nne wamepoteza maskani zao.Majadiliano ya amani yaliofanywa Naivasha nchini Kenya yamekwama tangu mwisho wa mwezi Oktoba.Mazungumzo hayo lakini yamepangwa kuendelea Novemba 30.