Jimmy Carter si ruhusa Gaza
15 Aprili 2008Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter amekataliwa ruhusa na Israel ya kutembelea mwambao wa Gaza unaotawaliwa na chama cha Hamas.Hatahivyo, amehakikisha tena kwamba ana azma ya kukutana na kiongozi wa Hamas anaeishi uhamishoni mjini Damscus,Syria.Majeshi ya Israel mapema leo yaliingia kwa magari ya aina ya vifaru,buldoza na kufyatuliana risasi na wapalestina.
►◄
Akiendelea na ziara yake ya Mashariki ya Kati,Jimmy Carter,mshindi wa nishani ya amani ya Nobel mwaka 2002 na alietunga mkataba wa amani wa 1979 kati ya Misri na Israel ,amesema Israel imemkatalia ruhusa ya kuzuru Gaza ingawa alipendelea sana kuzuru huko."niliomba ruhusa kwenda Gaza,lakini nilikataliwa."
Jimmy Carter aliwaambia maripota mjini Ramallah kabla kukutana na waziri mkuu wa Mamlaka ya Ndani ya wapalestina Salam Fayyad.
ZiarA YA SIKU 9 YA RAIS CARTER MASHARIKI YA KATI IMEKOSOLEWA VIKALI TANGU NA MAREKANI YENYEWE HATA NA MSHIRIKA WAKE Israel inayoudhibiti mlango wa kuingilia mwambao wa Gaza.
Zote mbili zimemtaka Jimmy Carter kutosonga mbele na mpango wake wa kukutana uso kwa uso na Bw.Khaled Meshaal,kiongozi wa Hamas anaeishi uhamishoni mjini Damascus,Syria.
Chama cha Hamas kilichonyakua mamlaka huko gaza hapo juni,mwaka jana baada ya kuvitimua vikosi vya ulinzi vitiifu kwa rais Mahmud Abbas,kinaangaliwa ni chama cha kigaidi na Marekani,Israel na hata umoja wa Ulaya.
"Nitafanya kila juhudi kumfanya awafik suluhisho la amani tangu na Israel hata na chama cha Fatah." alisema Jimmy Carter.
Rais huyo wa zamani wa Marekani na mkewe Rosalyn Carter ,waliweka koja la maua katika kaburi la marehemu Yasser Arafat huko Ramallah.
Koja hilo la maua liliandikwa jina "Rais na bibi Carter."
Rais carter hatahivyo, amepangwa kuhudhuria leo karamu ambamo makamo wa zamani wa waziri mkuu na Kiongozi wa hadhi ya juu wa Hamas ukingo wa magharibi Nassereddin al-Shaer atahhudhuria.
Rais Carter alisema juzi jumapili kwamba viongozi wa Israel wamekataa kuonana nae wakati wa ziara yake hii itakayomchukua pia Jordan,Syria,Saudi Arabia na Misri.
Jimmy Carter amewakasirisha waisraeli kwa kitabu chake cha 2006 ambamo amelinganisha kukaliwa ardhi za wapalestina huko ukingo wa magharibi kuwa sawa na zile siasa za ubaguzi na mtengano-aparthied za iliokua Afrika kusini.
Vikosi vya Israel viliimngia hii leo kusini mwa mwambao wa Gaza na kuwasaka wapalestina wanao waanmdama. Wakafyatuliana risasi na miripiko iliowajeruhi si chini ya watu 5.Kiasi cha magari 20 ya aina ya vifaru ya Israel yakifuatana na mabldoza pamoja na ndeg2 2 za helikopta zenye mizinga yaliingia hadi maili 1 ndani ya eneo linalomilikiwa na Hamas karibu na kivuko cha Kissufim.Waliipekua shule moja na nyumba nyengine katika mtaa wa Al-Qarara na Wadi Al-Saqla.Hapo wakafyatuliana risasi na wanamgambo wa kipalestina .