1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Jeshi la Urusi lakiri Ukraine iliwashika pabaya Kursk

12 Agosti 2024

Urusi imekiri jana Jumapili kuwa wanajeshi wa Ukraine waliingia ndani kabisaa ya mkoa wa Kursk, katika shambulio ambalo afisa wa juu wa Ukraine amesema lililenga kuivuruga Urusi na kuvitatiza vikosi vyake.

https://p.dw.com/p/4jMZM
Urusi Kursk | Uharibifu baada ya shambulio la roketi la Ukraine
Urusi, Kursk | Uharibifu baada ya shambulio la roketi la UkrainePicha: Ilya Pitalev/Sputnik/IMAGO

Na baadae Jumapili, kila nchi iliilaumu nyingine kwa moto uliotokea kwenye mtambo wa nyuklia wa Zaporizhzhia unaokaliwa na vikosi vya Urusi kusini mwa Ukraine, ingawa kila upande, pamoja na shirika la nyuklia la Umoja wa Mataifa, walisema hakukuwa na ishara ya kuvuja kwa nyuklia.

Kyiv alipeleka maelfu ya wanajeshi katika shambulio la kustukiza ndani ya Urusi, baada ya miezi kadhaa ya kusonga mbele kwa taratibu kwa vikosi vya Urusi katika mikoa ya mashariki.

Urusi Ukraine| Watu waliookolewa baada ya shambulio la Kursk
Watu wapatao 76,000 walihamishwa Kursk kufuatia uvamizi wa Ukraine.Picha: Ilya Pitalev/SNA/IMAGO

Shambulio hilo ambalo hivi sasa liko katika siku yake ya saba, lilionekana kuistukiza Kremlin, ambapo jeshi la Urusi lilitumia wanajeshi wa kiba, vifaru, mashambulizi ya angani na droni katika juhudi za kulizima.

Hapo jana jeshi la Urusi lilionekana kukiri kwamba Ukraine imefanikiwa kupenya kwenye ardhi yake kwa umbali wa hadi kilomita 30.

Katika taarifa ya kila siku katika mkoa wa Kursk, wizara ya ulinzi ilisema ilikuwa imezuwia majaribio ya vikosi vya Ukraine kuingia zaidi eneo la Urusi kwa kutumia magari ya kivita.