1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ukraine limesema limedungua droni 41 za Urusi

8 Januari 2025

Jeshi la Ukraine limesema Urusi imeishambulia ardhi ya taifa hilo kwa droni 64, lakini pia katika kipindi hichohicho upande wa Urusi unasema Ukraine imevurumisha droni kadhaa katika miji ya Saratov na Engels.

https://p.dw.com/p/4owAI
Ukraine Krieg | Mobilität der ukrainischen Armee in Richtung Kurachowo fortgesetzt
Wanajeshi wa Ukrein wakitayarisha kivita baada ya kufanya mashambulizi kadhaa, kuelekea Kurakhove, Ukraine, Mkoa wa Donetsk Desemba 4, 2024.Picha: Diego Herrera Carcedo/Anadolu/picture alliance

Ndani nchini Ukraine jeshi la Ukraine linasema kati ya droni hizo 64 za Urusi 41 zimepanguliwa, huku 22 zikishindwa kufika katika maeneo yaliolengwa. Mamlaka katika mji wa Kyiv inasema mabaki ya droni zilizodunguliwa yaliangukia katika maeneo ya makazi binafsi ya mji wa Kyiv. Kumetoka uharibifu wa majengo hayo ikiwemo madirisha pasipo athari kwa binaadamu.

Kwa upande wa Urusi mashambulizi ya droni za Ukraine yapiga miji ya Saratov na Engels, ambapo Urusi ina kambi yake ya anga ya ndege za kimkakati za kivita. Gavana wa eneo hilo, Roman Busargin amesema miji hiyo miwili ilikumbwa na shambulio kubwa la ndege zisizo na rubani na kulikuwa na uharibifu katika eneo la viwanda. Ingawa hakugusia kama kambi ya jeshi la anga ya Engels kama ilishambuliwa pia.

Taarifa ya namna kiwanda kilivyowaka moto

Busargin amesema kulitokea  moto katika kiwanda kimoja kilichoshambuliwa, ingawa hakukuwa na hakuna taarifa za majeruhi au vifo.Vyombo vya habari vya Urusi vyenye mawasilianao na mifumo ya kiusalama ya taifa hilo vimechapisha picha zinazoonyesha moto mkubwa na kusema watu katika maeneo hayo wametoa taarifa ya kutokea miripuko mingi.

Ukraine Kurachowe | Russisches Militär meldet Einnahme ukrainischer Kleinstadt
Barabara kuu imefunikwa na vifusi kutoka kwa majengo ya makazi yaliyoharibiwa baada ya shambulio la Urusi.Picha: Anton Shtuka/AP/dpa/picture alliance

Kambi ya Engels ni makazi ya ndege za kivita za masafu marefu ambayo ni sehemu ya vikosi vyake vya kimkakati vya nyuklia. Iko umabli wa kilometa 730 kusini mashariki mwa Moscow na mamia ya kilomieta kutoka mpaka wa Ukraine.

Jaribio la mashambulizi ya kambi ya kijeshi ya Engels

Rekodi zinaonesha kuwa Ukraine iliwahi  kushambulia kambi hiyo hapo awali. Desemba 2022, Wanajeshi watatu wa jeshi la anga la Urusi waliuawa baada droni kudunguliwa eneo hilo.

Nje ya eneo la mapambano, Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema anapanga kujadili juhudi za kumaliza vita vya Urusi huko Ukraine na Rais wa Urusi Vladimir Putin. Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Florida, Trump alipendekeza mkutano huo ufanyike baada kuingia ofisini rasmi Januari 20.

Katika mkutano wake huo na waandishi wa habari, alionesha matumaini ya kwamba vita hivyo vitamalizika ndani ya miezi sita. Ikumbukwe tu, kawamba wakati wa kampeni yake, Trump mara nyingi alisifu uhusiano wake na Putin na kudai kuwa anaweza kumaliza vita nchini Ukraine "ndani ya masaa 24."

Soma zaidi:Urusi, Ukraine zaendelea kukabiliana vikali Kursk

Serikali ya Ukraine inahofia kwamba pale ambapo Trump atakapoingia madarakani Januari 20, misaada ya Marekani kwa taifa hilo itapunguzwa kwa kasi. Katika hotuba yake ya Mwaka Mpya, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alitoa wito kwa Marekani kutopunguza usaidizi kwa Ukraine.

Vyanzo: RTR/DPA