1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yaushambulia uwanja wa ndege Urusi

9 Agosti 2024

Jeshi la Ukraine limesema limeushambulia usiku wa kuamkia leo uwanja wa ndege wa jeshi la Urusi mjini Lipetsk, karibu kilomita 380 kutoka mpaka wa Urusi na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4jIQ9
Russisches Sukhoi Su-25-Düsenflugzeug
Picha: pSergei Bobylev/dpa/ icture alliance

Mkuu wa jeshi la Ukraine ameandika kwenye mtandao wa Telegram kuwa, shambulio hilo limesababisha uharibifu mkubwa ikiwemo kuharibu ghala la mabomu ya kuongozwa.

Ukraine imeeleza kuwa, ndege za kijeshi za Urusi chapa Su-34, Su-35 na MiG-31 zilikuwepo kwenye uwanja huo wa ndege ulioshambuliwa.

Gavana wa eneo la Lipetsk Oblast, Igor Artamonov, amesema kumefanyika shambulio la droni katika eneo hilo huku vyombo vya habari vya Urusi vikiripoti kuwepo kwa moto katika uwanja wa ndege wa kijeshi.

Gavana huyo amefuta baadhi ya hafla za umma zilizokuwa zimepangwa kufanyika katika eneo hilo na kuagiza watu wanaoishi karibu na uwanja huo wa ndege kuhama.