1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Marekani lawaua wanamgambo 37 nchini Syria

Josephat Charo
30 Septemba 2024

Kamandi kuu ya jeshi la Marekani, CENTCOM, imelieleza kundi la Hurras al-Din kama mshirika wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda nchini Syria lenye malengo ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/4lDUS
Kikosi cha jeshi la Marekani kikiwa katika operesheni nchini Syria.
Kikosi cha jeshi la Marekani kikiwa katika operesheni nchini Syria.Picha: Jensen Guillory/Planetpix/ZUMA Wire/picture alliance

Vikosi vya jeshi la Marekani vinasema vimefanya mashambulizi mawili ya kutokea angani nchini Syria na kuwaua wanamgambo 37 wa kiislamu, wakiwemo viongozi wa vyeo vya juu wa makundi ya kigaidi ya dola la kiislamu na Hurras al-Din, ambalo ni mshirika wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaeda.

Kamandi kuu ya jeshi la Marekani CENTCOM imeripoti jana Jumapili kwamba shambulizi kubwa la kutokea angani mnamo Septemba 16 katika kambi ya mafunzo ya kundi la dola la kiislamu katikati mwa Syria liliwaua wapiganaji wapatao 28, wakiwemo maafisa kiasi wanne wa ngazi za juu.

Kamandi hiyo aidha imesema shambulizi lengne la kutokea angani mnamo Septemba 24 kaskazini magharibi mwa Syria liliwaua magaidi tisa, akiwamo Marwan Bassam 'Abd-al-Ra'uf, kiongozi wa cheo cha juu wa kundi la Hurras al-Din aliyekuwa na dhamana ya kusimamia operesheni za kijeshi kutokea Syria.