1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Jeshi la Marekani lahitimisha mchakato wa kuondoka Niger

17 Septemba 2024

Marekani imesema imemaliza kuwaondoa wanajeshi wake nchini Niger. Mchakato huo ulifanyika kwa awamu, limesema jeshi la Marekani jana Jumatatu kupitia Kamandi yake ya Uratibu Barani Afrika.

https://p.dw.com/p/4khB6
Niger Niamey 2024 | maafisa wa Marekani wa Marekani na Niger
Maafisa wa ngaz za juu wa jeshi la Marekani na Niger wakiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kabla ya kutangaza rasmi kuondoka nchini NigerPicha: ISSIFOU DJIBO/EPA

Kwa muongo mmoja uliopita, wanajeshi wa Marekani wametoa mafunzo kwa vikosi vya Niger na kusaidia kukabiliana na ugaidi wa makundi ya Dola la Kiislamu na al Qaeda katika eneo hilo.

Serikali ya kijeshi ya Niger mnamo mwezi Aprili iliagiza Marekani kuondoa wanajeshi na watumishi wengine wapatao 1,000 nchini humo. 

Kabla ya mapinduzi, Niger ilikuwa mshiriki mkubwa wa Marekani katika vita dhidi ya uasi katika ukanda wa Sahel, na kusababisha vifo vya maelfu na wengine mamilioni kukimbia makazi yao.

Washington inaangazia mpango mbadala katika eneo la Afrika Magharibi lakini mchakato huu unakwenda taratibu.