1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Israel lashambulia wanamgambo na miundombinu Gaza

31 Oktoba 2023

Jeshi la ardhini la Israel linasema limewashambulia wanamgambo wa Hamas na miundo mbinu kaskazini mwa Ukanda wa Gaza wakati vita kwenye ukanda huo vikiingia wiki ya nne.

https://p.dw.com/p/4YDx5
Israel Palästina I Gaza
Ukanda wa Gaza ukiendelea kushambuliwa na makombora ya Israel, Jumatatu ya 30 Oktoba 2023.Picha: Ismael Mohamad/UPI/IMAGO

Jeshi la Israel limesema karibu watu 800,000 wamekimbia eneo hilo tangu vita vilipoanza zaidi ya wiki tatu zilizopita, hata wakati ndege za kivita zikiendelea kufanya mashambulizi ya angani katika Ukanda huo uliozingirwa.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel amekataa miito ya kusitisha mapigano na kwa mara nyingine akaapa kuuvunja uwezo wa kundi hilo kuitawala Gaza au kuitishia Israel kufuatia uvamizi wake wa Oktoba 7.

Soma zaidi: Gaza:Hakuna njia ya kutoka kwa Wapalestina wenye uraia pacha

Hamas imewaachia mateka wanne, na imesema itawaachia wengine kwa kubadilishana na maelfu ya wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa na Israel.

Israel imekataa pendekezo hilo.